Published On: Sat, Jul 8th, 2017
Sports | Post by jerome

Lukaku kufanyiwa ukaguzi wa kimatibabu Old trafford

Share This
Tags

Romelu Lukaku anatarijiwa kufanyiwa ukaguzi wa kimatibabu na Manchester United baada ya kukubali kuilipa Everton kitita cha pauni milioni 75 ili kumsajili mshambuliaji huyo wa Ubelgiji.

Makubaliano hayo ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, yalioripotiwa awali na BBCsport siku ya Alhamisi yanaaminika kushirikisha marupuru mengine ya pauni milioni 15.

United imesema kuwa wamefurahishwa na makubaliano hayo na kwamba usajili wake utafanywa tu baada ya kufanyiwa ukaguzi wa matibabu na makubaliano ya kibinafsi.

Chelsea ilikuwa imefikisha kiwango kilichokuwa kikitolewa na Manchester United lakini wakaonekana kushindwa kumsajili mchezaji wao wa zamani.

The Blues hawakuwa tayari kufikisha kiwango kilichotakiwa na ajenti wa mchezaji huyo Mino Riaola iwapo mchezaji huyo angeelekea Old Trafford.

Tangazo jingine litafanywa katika muda wowote, iliongezea United.

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho alikuwa mkufunzi wa Chelsea wakati timu hiyo ilipomuuza mchezaji huyo kwa Everton kwa pauni miloni 28 mnamo mwezi Julai 2014.

Mbelgiji huyo alifunga mabao 25 katika ligi ya Uingereza msimu uliopita na Manchester United wamekuwa wakitaka kumsajili msimu wote uliopita.

United wanaharakisha usajili wa mchezaji huyo kabla ya kuondoka kuelekea Marekani kwa maandilizi ya msimu ujao siku ya Jumapili.

Wayne Rooney hatarajiwi kuwa miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha United kwa ziara hiyo kwa kuwa anatarajiwa kurudi Everton kwa uhamisho wa bure.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>