Published On: Wed, Jul 5th, 2017
Sports | Post by jerome

Lacazette amefuzu vipimo vya kitabibu kwenye klabu ya Arsenal

Share This
Tags

Mshambuliaji wa Lyon Alexandre Lacazette amekamilisha ukaguzi wa kimatibabu kabla ya kujiunga na Arsenal kwa kitita cha rekodi ya pauni milioni 45.

The Gunners ilikuwa imetoa kitita cha chini lakini kikakataliwa na hivyo basi kuendelea na mazungumzo.

Kitita hicho cha hadi pauni milioni 52 kitapita kile alichonunuliwa Mesut Ozil kutoka Real Madrid cha pauni milioni 42.4 2013.

Lazazette alikuwa wa pili kwa idadi ya mabao katika ligi ,Msimu uliopita akiwa na mabao 28.

Amefunga mabao 129 katika mechi 275 katika mashindano yote tangu alipoanza kuchezeshwa katika timu kikosi cha kwanza 2009-10.

Alishinda kwa mabao na mshambuliaji wa PSG Edison Cavani aliyefunga mbao 35.

Lacazzette ambaye ameichezea Ufaransa mara 11 amehusishwa na vilabu kadhaa vikuu na alitarajiwa kujiunga na Atletico Madrid.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>