Published On: Sat, Jul 22nd, 2017

Igunga yakabiliwa na uhaba wa chakula

Share This
Tags

Mpunga na Mahindi hutegemewa sana na wananchi wa wilaya ya Igunga kama zao kuu la chakula na Biashara.

Lakini mwaka huu hali ni tofauti ukilinganisha na miaka mingine iliyopita  kutokana na wilaya hiyo kukumbwa na ukame uliosababisha wakulima wa wilaya hiyo kutovuna kama walivyotarajia.

Malale Mtaturu, Kilige John na Kulwa Maguja ni wakulima wa Malugala Igunga ambao wanasema hali ya maisha inazidi kuwa ngumu kwa kutokuwa na chakula cha kutosha baada ya mazao yao kukauka shambani.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Igunga Peter  Onesmo , anasema robo tatu ya wilaya hiyo inakabiliwa na ukame na wameshaanza kufanya jitihada za kuweza kuzisaidia familia ambazo zimekumbwa na uhaba wa chakula

Kutokana na hali hiyo,baadhi ya wananchi wameshauri njia pekee kwa sasa ya kuweza kuwasaidia ni kuwapatia mbegu bora zitakazoweza kuhimili ukame na magonjwa ili kuepusha hali hiyo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>