Published On: Tue, Jul 11th, 2017
World | Post by jerome

Idadi ya vifo kutokana na kipindupindu yafikia watu 713 nchini Yemen.

Share This
Tags

Shirika la afya duniani limefahamisha kuwa idadi ya watu walopoteza maisha kutokana na janga la ugonjwa wa kipindupindu nchini Yemen imeongezeka na kufikia watu 713.

Aidha WHO limeripoti kuwa takribani watu laki 3 na nusu kutoka katika maeneo 21 nchini humo wanasadikika kuambukizw maradhi hayo huku maambukizi yakienea kwa kasi katika mji mkuu Sana’a na miji ya jirani kama vile Hudayda, Amran na Hajja.

Chanzo kikubwa kilichopelekea maambukizi haya kusambaa kwa kasi ni mapigano makal, yanayoendelea nchini humo. Watu takriban milioni 3 nchini humo wanasadikika kutopata huduma ya maji safi kufuatia mapigano yanayoendelea.

Kuachwa kwa taka na kutokukusanywa kwa mpangilio kumepelekea uwepo wa mlipuko wa kipindupindu.

Wakati huohuo zaidi ya nusu ya wakazi wa nchi hiyo yenye jumla ya wakazi wapatao milioni 28, hawapati lishe bora na yakutosha. Watu milioni saba kati ya hao wapo katika hali mbaya ya baa la njaa.

Kwa mujibu wa shirika la watoto la Umoja wa Mataifa Unicef,takriban watoto milioni 1 na laki 3 wapo katika hatari ya kupata Nimonia.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>