Published On: Wed, Jul 12th, 2017
World | Post by jerome

China yafungua kituo cha kwanza cha kijeshi Djibouti

Share This
Tags

China imewatuma wanajeshi wake watakaohudumu katika kituo chake cha kwanza cha kijeshi nje ya nchi, kitakachokuwa nchini Djibouti.

Nafasi ya Djibouti kwenye ukingo wa Bahari ya Hindi imeongeza wasiwasi nchini India kuwa inaweza kuwa mojawapo ya washirika wa kijeshi wa China, ikiwa ni pamoja na Bangladesh, Manyamar na Sri Lanka.

China ilianza ujenzi wa kituo cha kijeshi nchini Djibouti mwaka jana ambacho kitatumiwa katika kuwasilisha vifaa kwenye meli zake za kivita zinazoshiriki katika operesheni za kulinda amani na za misaada ya kiutu hasa katika pwani za Yemen na Somalia.

Hiki kitakuwa kituo cha kwanza cha kijeshi cha China nje ya nchi, ijapokuwa China inakielezea kuwa ni kituo cha vifaa.

Shirika la habari la taifa Xinhua limesema katika ripoti fupi kuwa meli zilizowabeba askari wa Jeshi la Ukombozi la China ziling’oa nanga kutoka bandari ya kusini mwa China ya Zhanjiang kuelekea Djibouti.

Kamanda wa jeshi la majini Shen Jinlong alisoma taarifa kuhusu ujenzi wa kituo hicho nchini Djibouti lakini ripoti hiyo haikusema ni lini kituo hicho kitaanza operesheni zake.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>