Published On: Fri, Jul 14th, 2017
Business | Post by jerome

BIDHAA ZAENDELEA KUPITISHWA KIMAGENDO MPAKA WA SIRARI

Share This
Tags

Imebainika kuwa baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu mkoani mara, bado wanatumia mpaka wa sirali uliopo wilayani tarime katika njia zisizo rasmi, kupitisha bidhaa za chakula, dawa, vipodozi pamoja na vifaa tiba ambavyo havijasajiliwa kwa kutoka nchi jirani ya Kenya.

Wakizungumza wilayani bunda mara baada ya kuhitimisha zoezi la ukaguzi katika maduka, zahanati, hospitali pamoja na viwanda vya kusindika chakula katika wilaya zote za mkoa wa mara wakaguzi wa dawa toka mamlaka ya chakula kanda ya ziwa wamesema ukaguzi huo umebaini kuwepo kwa ongezeko kubwa la uingizwaji wa dawa sizizo sajiliwa katika maeneo ya Tarime, sirali, nyamongo na rorya.

 

Katika hatua nyingine VENANCE BULUSHI amewataka wananchi kuendelea kuta taarifa za bidhaa bandia baada ya kupata elimu ili waweze kuwachukulia hatua kali wahusika.

 

HASSAN LUBANGO ni mmoja wa wakazi wa mkoa wa mara kutoka wilayani bunda akatumia fursa hiyo kutoa wito kwa wafanyabiashara na serikali katika kudhibiti biadhaa hizo

Jumla ya bidhaa zinazokinzana na sheria za nchi zenye thamani ya zaidi ya milioni sita zimekamatwa katika wilaya zote za mkoa wa mara

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>