Published On: Fri, Jul 14th, 2017

AJIRA MPYA ZAIDI YA ELFU SITINI ZIKIWEMO ZA DHARURA ZATANGAZWA

Share This
Tags

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ANGELA KAIRUKI amesema hatma ya watumishi walioghushi vyeti kulipwa au kutolipwa mafao yao bado haijajulikana huku akitangaza ajira mpya zaidi ya Elfu Sitini zikiwemo za dharura.

Tangu kuondolewa kwa watumishi wa umma zaidi ya Elfu tisa wenye vyeti vya kughushi malalamiko yamekuwa ni kuwepo kwa upungufu wa watumishi hasa katika sekta ya afya swali ambalo limepatiwa majibu.

Akiwa katika ziara ya kuzungumza na watumishi wa Umma na kupokea malalamiko katika wilaya ya Kinondoni Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ANGELA KAIRUKI anaeleza hatma ya watumishi walioondolewa kwenye ajira.

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni ALI HAPI akaeleza namna uhaba wa watumishi unavyosababisha wafanye kazi nyingi kuliko uwezo wao.

Katika ziara yake Waziri KAIRUKI amesema watumishi wenye elimu ya Darasa la saba walioajiriwa baada ya Mei, 20 mwaka 2004 watachukuliwa hatua huku akiweka wazi kuwa watumishi wanaostaafu wataondolewa kwenye orodha ya malipo muda huohuo.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>