Published On: Fri, Jun 16th, 2017

ZAIDI YA WALIMU 3,000 WA SAYANSI NA HISABATI WAPATA AJIRA MWAKA HUU

Share This
Tags

Zaidi ya Walimu 3,000 wa Masomo ya Sayansi na Hisabati wameajiriwa Mwaka 2017, ambao Tayari Serikali imekwisha Wapangia Vituo vya Kazi Katika Shule Mbalimbali Zilizopo hapa Nchini.

Kulingana na Maelezo ya Naibu Waziri wa Tamisemi SELEMAN JAFO, Ajira hizi zimetolewa Kwa walimu waliohitimu Mafunzo ya Kada hiyo Mwaka 2015 / 2016.

Akijibu Swali la Mbunge wa Mbagala JAMAL KASSIM, Naibu Waziri JAFO amesema  Mpango wa Serikali ilikuwa Kuajiri Walimu 4,129. Wakati huo huo Serikali imesema itaendelea Kuboresha Maslahi na Stahiki Mbalimbali Kwa Maofisa na Askari Kwa Kuzingatia hali ya Maisha ya Wakati Husika na Uwezo wake Kifedha Kumudu Kulipa Stahiki hizo.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt HUSSEIN MWINYI akijibu Swali la Mbunge wa Micheweni HAJI KHATIB KAI. Mbunge wa Mbeya Mjini JOSEPH MBILINYI akiuliza Swali la Nyongeza Kwa Dkt MWINYI alitaka Serikali ilithibitishie Bunge hilo Kama Serikali inao Mpango wa Kuzifuta Posho hizo.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>