Published On: Fri, Jun 16th, 2017

YALIOJIRI DODOMA

Share This
Tags

 

 

Serikali imesema inafanya mapitio ya majukumu ya watumishi wote wakiwemo walimu ili kuboresha maslahi yao kwakuzingatia uzito wa kazi kwani taifa lolote linategemea watumishi katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Pamoja na hilo pia viongozi wote wakiwemo wabunge wametakiwa  kujenga utaratibu wa kuwapa motisha watumishi ili kuwapa ari ya kufanya kazi kwa ufanisi na kulitumikia taifa.

Naibu waziri wa nchi ofisi ya rais TAMISEMI SELEMANI JAFO ametoa rai hiyo Bungeni wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum GRACE TENGEGA aliyeuliza serikali inampango gani wa kuboresha maslahi ya walimu kama ilivyokuwa miaka ya nyuma ili kutoa elimu bure yenye ubora.

Katika swali lake la nyongeza baada ya majibu ya naibu waziri  GRACE TENDEGA aliuliza ili viongozi waweze kutoa motisha kwa watumishi je serikali ipo tayari kurudisha vyazo vya mapato kwa halimashauri.

Naye mbunge wa viti maalum SUZAN LYMO wakati akiuliza swali la nyongeza  amesema serikali haioni wanafunzi wanaendelea kufundishwa na vutabu vyenye makosa swali ambalo limejibiwa na waziri wa elimu na sayansi na technologia JOYCE NDALICHAKO.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>