Published On: Sat, Jun 17th, 2017

Wauguzi mbaroni kwa kifo cha mtoto wa miezi minne

Share This
Tags

POLISI Mkoani Singida inawashikilia wauguzi wawili kwa kusababisha kifo cha mtoto wa miezi minne aliyelazwa hospitali ya Wilaya Manyoni, kutokana na tatizo la moyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa Singida, Deborah Magiligimba, amesema wauguzi hao ni Salma Mkoko na Spesioza Mushumbusi, ambao walisahau kuutoa mpira waliomfunga mtoto Cesilia Dastan,wakati wanamwongezea drip ya maji hali iliyosababisha mkono wake wa kulia kuvimba.

Kutokana na kifo hicho, kamanda Magiligimba, ametoa wito kwa wauguzi kuwa makini na kazi zao ili kuepuka malalamiko kutoka kwa jamii.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>