Published On: Tue, Jun 13th, 2017

Watumishi wa uma kuendelezwa

Share This
Tags

Serikali imesema itaendelea kuwaendeleza watumishi wa uma nchini kwani ni rasilimali muhimu katika kufanya utekelezaji wa majukumu na malengo yake ili kujenga nguvu na mafanikio kwa taifa.

Waziri wa nchi ofisi ya rais utumishi na utawala bora ANGELA KAIRUKI ametoa taarifa hiyo wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum RUTH MOLLEL aliyeuliza mkakati wa serikali wa kuwapa motisha watumishi wa umma.

Waziri kairuki amesema kuwa mbali na kuwaendeleza watumishi pia ipo mikakati mbalimbali ambayo imefanyika ikiwa ni pamoja na kupunguza kiwango cha kodi yamapato kwenye mshahara yao

Katika hatua nyingine wakati akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa bunge waziri KAIRUKI amesema Tanzania inaungana na nchi nyingine dunia ni kuadhumisha wiki ya utumishi wa uma kwa kufanya ziara za kuwatembelea watumishi na kusikiliza kero.

Kauli mbiu ya mwaka huu kwa bara la afrika ni kuimarisha ushirikiswaji wa jamii katika kutoa huduma vijana washirikishwe kuleta mabadiliko barani afrika ambapo wiki ya maandimisho inaanza tarehe 14 hadi tarehe 23 june.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>