Published On: Sat, Jun 17th, 2017

Watu 89 wafariki migodini

Share This
Tags

Wachimbaji 89 wamepoteza maisha, katika matukio 42 ambayo yamesababisha zaidi ya majeruhi 39 mkoani geita kwa mwaka 2008 hadi 2017 kutokana na usalama mdogo kwenye machimbo ya madini.

Mkaguzi wa Migodi kutoka Ofisi ya Madini Mkoa wa Geita Ali Maganga ambaye kwa sasa amehamishiwa Mkoani Kagera,anasema takwimu hizo zimekuwa zikiongezeka kila mwaka.

Kutokana na hali hiyo, wadau wa sekta ya madini  akiwemo Kamishina Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa YAHAYA SAMAMBA wanakutana mkoani Geita  kujadili namna ya kutatua changamoto hizo, huku shirika lisilokuwa la kiserikali la Plan International likipinga vikali ajira za watoto migodini.

Kupitia mafunzo hayo Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga,  ametoa rai kwa Ofisi ya Madini Kanda ya Ziwa pamoja na Geita, kuhakikisha wanatoa mafunzo ya mara kwa mara kwa wachimbaji wadogo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>