Published On: Fri, Jun 9th, 2017
Sports | Post by jerome

WASHIRIKI WA MASHINDANO YA UMITASHUMTA  YAKABIDHIWA VIFAA

Share This
Tags

 

Ni uzinduzi wa Umitashumta kwa Mkoa wa Lindi ambapo washiriki wa mashindayo hayo , wanamepokea vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh mill 14  laki 296 na 160 kwa wanafunzi wa shule za msingi  wanao jiandaa na umitashumta kwa shule zote za msingi nchini kwa lengo la kufanya vizuri katika mashindano hayo huko jijini mwanza na hatimaye kurudi na ushindi nyumbani

Akiongea wakati wa kupokea vifaa hivyo kutoka katika mradi wa   gesi asilia nchini  katibu tawala wa mkoa wa lindi  Ramadhani Kaswa amesema wadau wanatakiwa wajitoe kikamilifu ili kusaidia michezo kwa kuibua vipaji  na kuinua michezo kwa mkoa wa lindi

Meneja  mawasiliano kutoka mradi wa  gesi asilia, Catherini Mbatia akawataka washiriki wa mashindano  hayo kutokuwa washiriki wa mashindano hayo tu, bali kuhakikisha   wanafunzi watakao pata nafasi katika kuwakilisha mkoa katika mashindano ya umitashumta kuhakikisha  wanarudi  na ushindi na kuutangaza mkoa wa lindi.

 

Mkoa wa lindi una shule za msingi zipatazo 496 na wanafunzi  laki 2 elfU 316 na  ambao baadhi yao wanaunda timu sita za michezo mbali mbali zitakazo wakilisha mkoa wa lindi katika umitashumta mashindano ambayo kitaifa yatafanyika  jijini Mwanza.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>