Published On: Mon, Jun 19th, 2017

WASAFIRISHA MIZIGO BILA KULIPA USHURU

Share This
Tags

 

Licha ya serikali kutoa mashine za kierektroniki kwa ajili kukusanyia mapato katika halmashuri hapa nchini ili kuokoa  fedha nyingi ambazo zimekuwa zikipotea bila utaratibu, hali hiyo imeendelea kujitokeza kwa kasi kwa kile kinachodaiwa kwamba wafanyabiashara husafirisha mizigo mingi bila kulipia ushuru

Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma JUMA MNWELE amesema fedha nyingi zinaendelea kupotea kutokana na wafanyabiashara wengi kushirikiana na watendaji wa kata na vijiji wasiokuwa waaminifu kukwepa kulipa tozo na kusema wamefanya zoezi maalum na kukamata magari yanayosafirisha mazao  ya mashambani bila kulipia

Hata hivyo baadhi ya madereva ambao walikataa kutaja majina yao wamelalamikia kitendo cha wenzao kukamatwa na kuwekwa mahabusu kwa sababu ya ushuru wakisema wao si wafanyabiashara na si kazi yao kuangalia ni mizigo kiasi gani ambayo haijalipiwa ushuru.

Katika zoezi hilo lililochukua  siku sita, shilingi milioni mbili zimekuwa zikiokolewa kila siku, ambapo mkurugenzi huyo ameahidi kuwachukulia hatua watendaji ambao wamekuwa si wakweli huku mmoja wao akisema hawezi kulizungumzia hilo maana yeye ana taratibu zake katika kazi.

Wakulima  na wafanyabiashara wadogo ambao huwa wanawauzia wafanyabiashara wakubwa wameitaka serika kukaa na watendaji wao ili kutoa maelekezo  kwa kuwa hata  sababu ya kuwepo kwa mashine za kukusanyia ushuru haionekani kuwa na matunda mazuri.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>