Published On: Tue, Jun 13th, 2017

Wanawake wa kiislam Shinyanga waaswa kusimamia elimu ya watoto wao

Share This
Tags

Wanawake wa kiislam wametakiwa kuhakikisha kuwa watoto wao wanapata elimu ya dunia na elimu ya akhera ili kuendana na hali halisi ya maisha ya sasa.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ametoa rai hiyo wakati akifungua kongamano la wanawake wa kislam wa msikiti wa Istighama na kusema ifike wakati kwa wanawake wa kiislamu kubadili mtanzamo wa maisha kwa kusimamia masomo ya watoto wao.

Aidha mkuu huyo wa wilaya amewataka akina mama hao kuweka mikakati ya pamoja ya kuhakikisha mtoto wa kike anasoma na kufikia malengo yake bila kujali itikadi za kidini.

Mkoa wa shinyanga ni miongoni mwa mikoa ambayo watoto wa kike wanaolewa katika umri mdogo kutokana na wazazi wao kuwaozesha mapema kwa tama ya kupata mali ikiwemo ng’ombe.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>