Published On: Mon, Jun 12th, 2017
Business | Post by jerome

WALALAMIKIA MAFUTA KUCHANGANYWA NA MAJI MTWARA

Share This
Tags

Watumia huduma za Nishati na Maji mkoani Mtwara wamewalalamikia baadhi ya huduma zinazotolewa na wamiliki wa vituo vya kujazia mafuta kwa kuchanganya mafuta na maji.

Watumiaji hao pia wameilalamikia Mamlaka ya Maji safi na maji Taka mjini Mtwara MTUWASA kwa kusambaza maji machafu kwa wateja.

Wakizungumza katika mafunzo ya wajibu na haki kwa watumiaji wa huduma za nishati na maji kwa wakazi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, baadhi ya madereva pikipiki za abiria maarufu kama bodaboda pamoja na wananchi wamesema tatizo la kugundua maji katika mafuta ya pikipiki limetokea zaidi ya mara moja, huku wengine wakihoji juu ya maji machafu yanayotoka katika mabomba.

Mkuu wa kitengo cha mitambo na usambazaji maji wa MTUWASA, LUKELO WANDELAGE amekiri wateja kufikiwa na maji machafu mabombani.

Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma za Nishati na Maji EWURA kupitia baraza la huduma za watumiaji wa nishati na maji EWURA CCC wameendesha Mafunzo ya wajibu na haki kwa watumiaji wa huduma za nishati na maji kwa wakazi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>