Published On: Tue, Jun 13th, 2017

Wakazi wa mkuranga walalamikia uchimbaji holela wa mchanga

Share This
Tags

Wakazi wa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani  wamemwomba Rais Dr. John Magufuli  kuingilia kati na kufuatilia mwenendo mzima wa  uchimbaji  holela wa madini ya mchanga  unaofanywa na baadhi ya watu kwa maslahi yao  binafsi.

Wakazi hao wanasema katika baadhi ya maeneo ya Mkuranga, kuna  shughuli za uchimbaji wa mchanga zikiendelea kufanyika hivyo serikali inapaswa kuzingatia  hilo na kuweka utaratibu mzuri ambao utaweza kuwanufaisha wakazi wa maeneo husika kwa kuzingatia sheria na taratibu.

Katika hatua nyingine wakazi hao wametoa pongezi kwa Rais Magufuli kwa uzalendo aliouonyesha kwa watanzania kwa kuunda Kamati Maalum ya Kuchunguza Masuala ya Kisheria na Kiuchumi Kuhusiana na Mchanga wenye Madini unaosafirishwa nje ya nchi.

Shaban Kifea ni miongoni mwa wazee maarufu Wilayani Mkuranga akizungumza kwa niaba ya wazee wenzake, anasema wameridhika na ripoti ambayo imekabidhiwa kwa Rais na ana imani itafanyiwa kazi ipasavyo na kuwawajibisha wale wote ambao wamehusika kulihujumu Taifa kwa maslahi yao binafsi.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>