Published On: Mon, Jun 19th, 2017
World | Post by jerome

WAGONGWA WAKITOKA MSIKITINI LONDON

Share This
Tags

Mshambuliaji amewagonga Waislamu waliokuwa wakitoka msikitini kaskazini mwa London na kumuua mtu mmoja na kuwajeruhi wengine 10 katika shambulizi la kigaidi.

Gari kubwa lililokodishwa liligonga kundi la waumini waliokuwa wakitoka sala za usiku muda mfupi baada ya saa sita za usiku katika msikiti wa Finsbury Park, moja ya misikiti mikubwa nchini Uingereza.

ABDULRAHMAN SALEH ALAMOUDI aliyekuwa katika eneo la tukio amesema kuwa dereva wa gari hilo alifika nje ya msikiti akiligongesha huku na kule gari hilo huku akipaza sauti akisema atawaua Waislamu wote.

Waziri mkuu wa Uingereza THERESA MAY amesema polisi wamethibitisha kuwa wanakichukulia kisa hicho kama shambulizi la kigaidi na kwamba ataongoza mkutano wa dharura wa kiusalama baadaye leo.

Watu wanane wamekimbizwa hospitalini wakiwa na majeraha huku wawili wakipokea matibabu katika eneo la tukio.

Polisi imesema mtu mmoja alitangazwa kufa papo hapo na dereva wa gari hilo mwenye umri wa miaka 48 alizuiwa na umma kabla ya kukamatwa na polisi.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>