Published On: Wed, Jun 14th, 2017

WACHIMBAJI WADOGO WA MGODI WA KITUNDA WAOMBA KUPATIWA KITUO CHA AFYA

Share This
Tags

WAKAZI wa kitunda wilayani Sikonge,wanaoishi kwenye machimbo ya dhahabu,wameomba kupatiwa huduma ya kituo cha Afya kutokana na wingi wao na  hivyo kuhatarisha usalama wao kiafya.

Baadhi ya wakazi wa mgodi huo,wamesema maisha yao yapo hatarini kutokana na kukosa kituo cha afya ambapo wanaweza  kupata magonjwa ya milipuko.

SIMON NGATUNGA ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Sikonge,anasema wanachukua hatua kadhaa kusaidia wananchi wanaoishi katika eneo hilo ambao wanazidi kuongezeka kila siku.

Eneo la Kitunda yalipo machimbo ya dhahabu,linavamiwa kwa wingi na wananchi wanaokwenda kutafuta maisha kwa kuchimba dhahabu ingawa mazingira kiafya sio mazuri.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>