Published On: Fri, Jun 9th, 2017

VIJANA WATAKIWA KUACHANA NA MATUMIZI YA MADAWA

Share This
Tags

 

 

IMEELEZWA  kuwepo  kwa vitendo vya matumizi ya madawa ya kulevya pamoja na ulevi wa kupindukia  hususan kwa baadhi ya vijana hapa nchini  vinachangia kwa kiasi kikubwa  kurudisha nyuma maendeleo ya Taifa kutokana  na kupoteza nguvu kazi kubwa ambayo ingeweza kutumika katika kuleta mabadiliko chanya ya kukuza uchumi wa viwanda  na kuondokana na wimbi la umasikini.

Kauli hiyo imetolewa na kiongozi wa Mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Amour Amour wakati wa kutembelea kituo cha vijana walioathirikika na utumiaji wa madawa ya kulevya cha Sober na  kuzungungumza na vijana kwa lengo la kuweza kutoa ujumbe dhidi ya athari zinazotokana na utumiaji wa madawa hayo ya kulevya.

Amour amesema kwamba kwa sasa serikali  ya awamu ya tano ipo katika mapambano makubwa dhidi ya dawa za kulevya  na kutoa elimu katika maeneo mbali mbali kwa lengo la kuweza kuwafanya vijana wote kuachana kabisa na madawa ikiwa sambamba na kuweka mipango mikakati ya kuwapatia matibabu wale wote walioathirika.

Nae Mkurugenzi wa kituo cha  sober Karim Banji amesema kwamba hadi sasa katika kuiunga mkono serikali katika kupambana na madawa ya kulevya   kituo hicho tayari kimesha wahudumia vijana  wapato 300 na kubainisha lengo la mradi  huo ni kuhakikisha  inawapatia huduma vijana  hao ili waweze kupona.

Awali mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga wakati wa kupokea mwenge huo wa uhuru  katika shule ya msingi mapinga  ukitokea Wilayani Kibaha amesema  kuwa  mwenge huo wa uhuru utatembelea  jumla ya  miradi 14 ya maendeleo katika halmashauri mbili za Wilaya ya Bagamoyo pamoja na halmashauri ya Chalinze  ambayo imegharimu  zaidi ya kiasi cha shilingi bilioni 100.

KAULI mbiu ya mbio za mwenge wa uhuru kitaifa kwa mwaka huu ambao bado unakimbizwa katika Mkoa wa Pwani  inasema Tanzania ya Uchumi wa viwanda inawezekana shiriki sasa katika ujenzi wake katika   kuleta maendeleo.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>