Published On: Tue, Jun 6th, 2017
Sports | Post by jerome

ULIMWENGU WA SOKA WAMUAGA CHEICK TIOTE

Share This
Tags

Ulimwengu wa soka umemuaga kiungo wa zamani wa timu ya Newcastle United Cheick Tiote aliyefariki dunia nchini China baada ya kuzimia wakati wa mazoezi.

Rafa Benitez, bosi wa zamani wa timu ya Uingereza ya Newcastle United, alimueleza Tiote aliyekuwa na umri wa miaka 30 kama mtaalamu wa kweli.

Tiote alijipatia jina katika clabu tofauti za Kiholanzi kabla ya kuhamia Newcastle mwaka 2010.

Mapema mwaka huu, alisaini mkataba na klabu ya China ya Beijing Enterprises.

Tiote alianza kucheza soka katika barabara za mjini Abidjan nchini Cote D’ivoire akiwa na umri wa miaka 10.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>