Published On: Tue, Jun 20th, 2017

Ujerumani na Tanzania zajidhatiti kuilinda Selous

Share This
Tags

Serikali za Tanzania na Ujerumani kwa pamoja zimezindua programu ya utunzaji wa mazingira na maendeleo katika hifadhi ya taifa ya Selous, SECAD, nchini Tanzania.

Hii ni miongoni mwa harakati za pamoja za mataifa hayo na asasi zisizo za kiraia za kutunza hifadhi hiyo na kukabiliana na vitisho vinavyoweza kuondoa hadhi yake kama moja ya eneo la kihistoria za turathi za dunia. 

Makubaliano hayo yalifikiwa Ijumaa iliyopita kati ya Waziri wa maliasili na utalii wa Tanzania Jumanne Maghembe na balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Egon Kochanke.

Programu hiyo inafadhiliwa na benki ya maendeleo ya Ujerumani ya KfW kwa niaba ya serikali ya Ujerumani na itatekelezwa na wizara ya maliasili na utalii, kwa kushirikiana na mamlaka ya hifadhi za wanyamapori, taasisi ya kimataifa ya hifadhi za uoto wa asili, WWF na asasi inayojihusisha na bustani za wanyama ya Frankfurt, FZS.

Waziri Maghembe alipozungumza kwenye uzinduzi huo uliofanyika eneo la Matambwe katika hifadhi ya Selous, amesema wanaukubali kwa kiasi kikubwa mpango huo wa serikali ya Ujerumani wa kulinda hifadhi hiyo.

Amesema hatua hiyo inatokana na mpango huo kuwa na msingi imara wa kulinda rasilimali za asili kwa faida ya taifa hilo na urithi wa asili kwa Tanzania.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>