Published On: Mon, Jun 12th, 2017

UJENZI WA BWENI KUWAPA NAFUU WANAFUNZI TANGA

Share This
Tags

Wanafunzi wa  Sekondari ya Kilale  mjini Tanga  sasa wataondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kutoka nyumbani kwenda shuleni  baada ya  wananchi wa kata ya Kilale kuamua kujenga bweni kwa nguvu zao ili kuwakomboa vijana hao kielimu.

Diwani wa kata hiyo MWAGILO SALEHE ADAMU amesema lengo la ujenzi huo ni kuwakwamua wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Kilale  ambapo baadhi yao hushindwa kumaliza masomo kutokana na kutembea umbali mrefu kutokana na vikwazo wanavyokutana navyo njiani ukiwemo ujauzito.

Aidha walimu wa shule hiyo wamekiri kuwepo kwa changamoto nyinginezo kwa wanafunzi ikiwemo kukosa masomo kutokana na kutofika darasani kwa wakati hali inayoshusha kiwango cha ufaulu shuleni hapo.

Hata hivyo  bweni hilo litakapokamilika  litakuwa na  jumla ya vyumba vyenye uwezo  wa kulaza wanafunzi wa kike 200  huku juhudi za kujenga bweni la wanafunzi wa kiume zikiwa mbioni.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>