Published On: Tue, Jun 13th, 2017
Business | Post by jerome

Uganda na Tanzania kujenga reli yenye uwezo wa kuendeshwa na umeme

Share This
Tags

Uganda na Tanzania zimeamua kujenga reli yake ya kisasa yenye uwezo wa kuendeshwa na umeme na kuanza kutumia umeme kwenye treni zake pindi tu watapokuwa na umeme wa kutosha.

Mratibu wa mradi wa SGR wa Uganda Kasingye Kyamugamba amesema wameamua kuwezesha treni yao kuendeshwa kwa umeme kwani miradi inayoendelea kwa sasa ya Karuma na Isimba itazalisha umeme wa kutosha

Nchini Kenya aidha waziri wa uchukuzi nchini humo James Macharia amesema baadaye watatumia umeme kuendesha treni zake mpya kwa gharama ya dola milioni $480 ili kuweka miundo mbinu inayohitajika.

Tayari reli ya Kenya ya kisasa kutoka Mombasa hadi Nairobi ya kilomita 472 inahudumu na awamu ya pili ya ujenzi wa reli kuelekea Naivasha inatarajiwa kuanza.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>