Published On: Wed, Jun 14th, 2017

UELEWA MDOGO KATIKA JAMII KUHUSIANA NA UCHANGIAJI DAMU

Share This
Tags

Uelewa ndogo katika jamii kuhusiana na uchangiaji damu ni sababu inayopelekea makundi ya watoto chini ya umri wa miaka mitano na mama  wajawazito  kutopata huduma stahiki na wakati mwingine kupoteza maisha  kutokana na hospital kutokuwa  na akiba ya kutosha ya damu  ya kuhudumia makundi hayo.

Wati watanzania wakiungana kwa pamoja ili kuweza  kuchangia damu, wakazi wa Bukoba pia wamejitokeza kuchangia damu na kueleza kuwa uzalendo  ndio njia pekee ya kuweza kunusuru maisha ya watu wenye uhitaji wa damu.

Mratibu Msaidizi wa kitengo cha damu Salama  mkoa wa  Kagera  Amos Bashweka anasema kuwa kimkoa wanakusanya unit elfu tatu za damu kila mwezi huku uhitaji ukiwa ni unit elfu nane,na kueleza kuwa hali hiyo inatokana na uelewa ndogo katika jamii na hofu ya kupata majibu baada ya kupima kwa ajili ya kuchangia damu.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>