Published On: Wed, Jun 14th, 2017

TAKWIMU ZA MAAMBUKIZI KUWA JUU ZASABABISHA WATU KUHOFIA KUCHANGIA DAMU MKOANI NJOMBE

Share This
Tags

Takwimu za maambukizi ya Virus vya Ukimwi mkoani Njombe zimedaiwa kusababisha wananchi kuogopa kujitokeza kuchangia damu katika vituo vya afya hali ambayo imepelekea bohari ya hospitali ya mkoa Kibena kuwa na upungufu wa damu.

Baadhi ya  wananchi wamesema wanashindwa kujitokeza kuchangia damu katika vituo vya afya na zahanati kutokana na hali ya maambukizi kuwa juu kimkoa hatua ambayo imedaiwa kuchangia mahitaji ya damu katika mkoa wa Njombe kuongezeka na kuhatarisha maisha ya wagonjwa .

Katika hatua nyingine wananchi hao wamesema wanakosa hamasa ya kujitokeza kuchangia damu katika hospitali ya Rufaa Kibena kwani licha ya kuchangia pindi wanapougua na kuhitaji msaada huo hulazimika kutafuta ndugu wakuchangia damu ili kupatiwa matibabu .

Dkt Wilfred Kyambile mganga mfawidhi Hospitali ya mkoa Kibena anasema mahitaji ya damu kwa mwaka katika hospitali hiyo ni zaidi ya uniti elfu 8 hivyo mwamko mdogo wa wananchi katika kuchangia unaweza kuhatarisha maisha ya wagonjwa wengi hususani majeruhi na akina mama wajazito .

Amesema kiasi kikubwa cha damu kinachopatika ni kutokana na jitihada zao za kuweka kambi katika taasisi za mbalimbali zikiwemo shule  huku hali ya wananchi kujitokeza kuchangia kwa siku ikionekana kuwa ndogo na wakati mwingine kukosekana kabisa.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>