Published On: Mon, Jun 19th, 2017

TABORA, UYUI, IGUNGA, NZEGA NA TINDE KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI

Share This
Tags

 

Serikali imesema mradi wa maji kutoka ziwa victoria kupitia mji wa kahama, umelenga kuwanufaisha wakazi wa Miji ya Tabora, Uyui, Igunga, Nzega, Tinde pamoja na vijiji 89 kupata huduma ya maji safi.

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi ISACK KAMWELWE amebainisha hayo leo Bungeni Mjini Dodoma Wakati akijibu Swali la Mbunge wa Bukene SELEMANI ZEDI.

Mhandisi KAMWELWE  amesema malengo ya mradi huo ni ya muda mrefu ambapo wananchi milioni 1.1 watakuwa na uhakika wa kupata huduma hiyo.

Naibu waziri huyo wa maji amesema serikali inakusudia kuanza kutekeleza mradi wa maji kwa ajili ya wananchi wa jimbo la pangani baada ya kupata ufadhili kutoka serikali ya india na uholanzi.

Ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum SAUM SAKALA.

Katika hatua nyingine serikali imelieleza bunge kwamba imefuta ushuru na tozo mbalimbali zilizokuwa zikitozwa kwa wafanyabiashara wasiokuwa rasmi ikiwemo mama lishe, wauza mitumba pamoja na wauzaji wa mazao ya kilimo.

JAFO amesema serikali pia haitawatoza kodi wafanyabiashara wadogo walio nje ya maeneo ya kibiashara ambao mitaji yao ipo chini ya shilingi 100,000.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>