Published On: Mon, Jun 19th, 2017
World | Post by jerome

SYRIA: NDEGE YETU YA KIJESHI ILIPANGA KULISHAMBULIA KUNDI LA IS

Share This
Tags

Jeshi la Syria limesema kuwa ndege yake ya kijeshi ilikuwa katika harakati za kushambulia kundi la Islamic State wakati iliposhambuliwa siku ya Jumapili.

Iimesema kisa hicho kitakuwa cha athari katika vita dhdi ya ugaidi.

Marekani imesema ilichukua hatua za kujilinda baada ya serikali ya Syria kuangusha mabomu karibu na wapiganaji wanaoungwa mkono na Marekani.

Kisa hicho kilitokea mji wa Ja’Din ambao unashikiliwa na vikosi vya Syrian Democratic Forces (SDF).

Wapiganaji wa SDF wanaoungwa mkono na muungano unaoongozwa na Marekani wamezingira ngome ya IS huko Raqqa.

Saa mbili kabla ya ndege hiyo kuangushwa, Marekani ilisema kuwa vikosi tiifu kwa raisi wa Syria BASHAR AL-ASSAD viliwashambulia wapiganaji wa SDF na kuwajeruhi kadhaa.

Mapema mwezi huu Marekani iliiangusha ndege isiyo na rubani ya seriikali ya Syria, baada ya ndege hiyo kushambulia vikosi karibu na kivuko cha mpaka cha Al-Tanf kwenye mpaka kati ya Syria na Iraq.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>