Published On: Wed, Jun 14th, 2017

Serikali yakiri Kwamba Bado Kuna Changamoto ya wanawake kuweza kumiliki Ardhi.

Share This
Tags

Serikali imekiri Kwamba Bado Kuna Changamoto ya Wanawake Kuweza Kumiliki Ardhi Hususani Maeneo ya Vijijini, Licha ya Kuwepo Kwa Matamko ya Kikatiba na Kisheria yanayolinda Haki ya Mwanamke Kumiliki Rasilimali hiyo.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ANGELINA MABULA ameliambia Bunge Mjini Dodoma Kwamba akina Mama wengi Wananyimwa fursa ya Kumiliki Ardhi Kwa Sababu ya Mila na Desturi za Baadhi ya Makabila Zinazowabagua.

Aidha Katika Kukabiliana na Changamoto ya Baadhi ya Makabila Kuendelea Kuwabagua Wanawake, Naibu Waziri huyo amesema Serikali imefanya Jitihada ya Kuboresha Sera ya Ardhi.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>