Published On: Thu, Jun 8th, 2017

SERIKALI KUWASILISHA BAJETI KUU BUNGENI LEO

Share This
Tags

Macho na masikio ya watanzania leo yanahamishiwa kwa muda mjini Dodoma wakati Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango atakapowasilisha bajeti kuu bungeni mjini humo kuanzia majira ya saa Kumi jioni.

Awali Wizara ya Fedha na Mipango iliwasilisha Bajeti ya kwanza ya Shilingi 29.5 trilioni.

Bajeti hiyo ndiyo iliyowafanya wachambuzi wa masuala ya uchumi, makundi ya biashara na wabunge kumtaka waziri huyo atangaze hatua mahususi za kuiokoa sekta binafsi na zitakazoharakisha ukuaji uchumi.

Wadau wanatarajia kuwa Dk Mpango, ambaye aliwahi kuwa mchumi mwandamizi katika Benki ya Dunia na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ataangalia kwa kina hali ya sasa ya uchumi na kutangaza hatua za kikodi zitakazozuia kupanda kwa gharama za maisha na wakati.

Pia anatarajiwa kuipa mkono sekta binafsi ili Serikali ifikie lengo lake kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

Mfumuko wa bei, ambao unahusishwa na kupanda kwa bei za vyakula, tayari umefika asilimia 6.4 kwa mwezi Aprili kutoka asilimia 5.1 mwezi kama huo mwaka jana.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>