Published On: Mon, Jun 12th, 2017

RIPOTI YA PILI YA MCHANGA WA MADINI YAWASILISHWA

Share This
Tags

Uwasilishaji wa ripoti ya pili ya makontena ya mchanga wa madini unaendelea Ikulu jijini Dar es salaam ambapo kamati ya wanasheria na wachumi iliyoundwa kuchunguza, inawasilisha ripoti hiyo wakati huu.

Kamati hiyo imebaini kuwa madini yaliyokuwa kwenye makontena hayakuwa makinikia bali madini ya aina mbalimbali.

Kamati imebaini pia kuwa Bulyanhulu na Pangea wanasafirisha makinikia bila kufuata utaratibu.

Kamati imebaini pia kuwa idadi na uzito wa madini hufichwa.

Kamati imebaini pia kuwa watumishi wa serikali, wamiliki wa kampuni za madini, na wapimaji wa madini wameisababishia serikali hasara kwa mujibu wa sheria ya madini kifungu cha 151.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>