Published On: Fri, Jun 2nd, 2017
Tech News | Post by jerome

RAIS MAGUFULI AZINDUA KITUO CHA NATIONAL INTERNET DATA CENTER

Share This
Tags

 

Rais Magufuli ametoa agizo hilo alipotembelea Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Kumbukumbu (National Internet Data Center) kilichopo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam na kisha kuzindua mfumo wa ukusanyaji wa kodi kwa njia ya kielektroniki.

Taarifa ya Kamishna Mkuu wa TRA Charles Kichere imebainisha kuwa  mpaka sasa ni kampuni tatu za simu ambazo ni TTCL, Halotel na Smart ndizo zimejiunga kutumia Mfumo huu na kwamba TRA na ZRB zinatarajia kampuni zote za simu, mabenki na taasisi mbalimbali kujiunga na mfumo wa e-RCS kabla ya mwisho wa mwaka 2017.

Pamoja na kutoa agizo hilo Rais Magufuli ametaka taasisi zote za Serikali zenye vituo vya kumbukumbu (Data Centers) kuoanisha vituo hivyo na amepiga marufuku kuendelea kuanzisha vituo vingine, na badala yake zitumie Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Kumbukumbu.

Nakisha Rais  akaitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzibana kampuni zote za simu ambazo hazijajiunga na soko la hisa la Dar es Salaam (DSE). naye  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akawahimiza Watanzania wote kulipa kodi ili kuinua uchumi. Mfumo wa ukusanyaji wa kodi kwa njia ya kielektroniki umetengenezwa na na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) kwa kutumia wataalamu wa ndani.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>