Published On: Tue, Jun 6th, 2017

Mwanaume anayedai kufunga kula miaka 28 mfululizo

Share This
Tags

Mwanamume mmoja raia wa Uturuki anadai kufunga kula kwa takriban siku  9,845  mfululizo bila ya kuacha hata siku moja .

Osman Ay ni mkaazi wa mkoa wa Kocaeli Magharibi mwa Uturuki.

Ay ni mwanamume wa umri wa miaka 50 sasa anasema kuwa amekuwa akikufunga kula tangu alipokuwa na miaka 21.

Bwana Ay anasema kuwa kilichomshawishi kuanza kufunga ni tukio moja ambapo alienda kujipima uzito wake na kutambua kuwa ana kilo 155.

Aliendelea kusimulia kuwa ndani ya miezi minne na nusu alikuwa amepoteza kilo 70.

Baada ya kugundua kuwa kufunga kunamfanya awe na afya bora zaidi aliendelea kufunga kila siku na kuzoea bila kupata taabu ya kuhisi njaa kwa kuwa mwili wake pia ulikuwa umeshazoea .

Ay katika kijiji chake pia anatambulika kwa jina la utani ‘Mwanamume anayefunga’

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>