Published On: Tue, Jun 13th, 2017
World | Post by jerome

Merkel atoa wito kupambana na umaskini Afrika

Share This
Tags

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani Jumatatu (12.06.2017) amehimiza kuwepo kwa uwekezaji zaidi barani Afrika kwamba ukuaji wa kiuchumi unahitajika kuupiga vita umaskini unaopelekea umma wa watu kukimbilia barani Ulaya.

Kansela Merkel amesema “Ukosefu wa matumaini ni mkubwa mno barani Afrika hapo tena bila ya shaka kutakuwepo na vijana wanaoamini kwamba inabidi watafue maisha mapya mahala kwengine duniani.Kwa hiyo iwapo tutashirikiana na nyinyi kuzisaidia nchi zenu hapo tutakuwa pia tunajiletea usalama zaidi sisi wenyewe binafsi na tunaweza kukomesha watu wanaofaidika kinyume na sheria kwa masahahibu ya wengine.”

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani akiufunguwa mkutano wa kundi la mataifa G20 lenye maendeleo ya kiuchumi na yale yanayoinukia kiuchumi duniani mjini Berlin hapo jana pamoja na viongozi 10 wa Afrika kama sehemu ya urais wa Ujerumani wa kundi la nchi hizo ambapo itakuwa na mkutano wake wa kilele mwezi ujao nchii Ujerumani.

Merkel amesema zaidi ya nusu ya Waafrika umri wao ni chini ya miaka 25 na idadi hiyo inatazamiwa kuongezeka maradufu kufikia katikati ya karne hii na kufanya ukuaji wa uchumi na ajira kuwa mambo muhimu sana.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>