Published On: Sat, Jun 17th, 2017
World | Post by jerome

Meli ya jeshi la Marekani yagongana na ya mizigo, wanajeshi 7 hawajulikani waliko

Share This
Tags

Mabaharia saba wa jeshi la majini pamoja na nahodha wao hawajulikani walipo na wengine wawili wamejeruhiwa baada ya meli ya kivita ya Marekani kugongana na meli ya mizigo ya Japan nje kidogo ya pwani ya Japan leo alfajiri.

Kwa mujibu wa msemaji mkuu wa walinzi wa mwambao wa Japan Yoshihito Nakamura, waokoaji wanaendelea na jitihada za kuwatafuta watu hao saba ambao inahofiwa walirushwa baharini wakati wa ajali au pengine wamekwama katika sehemu za meli hiyo ya kivita zilizoharibiwa na mgongano huo.

Hakuna mabaharia wa meli ya Japan walioripotiwa kujeruhiwa.

Kiwango cha uharibifu wa meli hiyo ya kivita ya Marekani kwa jina la Fitzgerald bado kinakadiriwa na tukio hilo lipo chini ya uchunguzi.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>