Published On: Tue, Jun 13th, 2017

Mbaroni kwa kujihusisha na mihadarati

Share This
Tags

Katika Kukabiliana na Vita Dhidi ya Dawa za Kulevya, Jeshi la Polisi Nchini limewatia Mbaroni Watuhumiwa 9,140 waliokuwa wakijihusisha na Biashara hiyo ya Mihadarati, Kufuatia Oparesheni Zilizofanywa na Jeshi Hilo Kuanzia Oktoba 2015 hadi April 2017.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi HAMAD MASAUNI ametoa Takwimu hizo Bungeni Mjini Dodoma, ambapo ameeleza Kuwa Watuhumiwa Wengine 14,410 kesi zao angali zinaendelea Mahakamani.

Naibu Waziri MASAUNI amebainisha hayo alipokuwa akijibu Swali la Mbunge wa Viti Maalum ZAINAB KATIMBA.

Masauni ameongeza Kuwa Jeshi la Polisi Nchini limeendelea na Programu ya Kuzuia Uhalifu Kwa Kuishirikisha Jamii Kwa Kutumia Sanaa na Michezo.

Wakati huo huo, Serikali imeelezea Kuwa na Utaratibu Mahususi wa Kuangalia Dawa, Vifaa tiba na Vitendanishi Kabla ya Kuvitoa Kwa Bohari Kuu ya Dawa na Kuvisambaza Kwenye Vituo vya Kutolea Huduma za Afya.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt HAMIS KIGWANGALLA ametoa Kauli hiyo Wakati akijibu Swali la Mbunge LUCIA MLOWE.

Katika Hatua Nyingine Wabunge Wameendelea Kuchangia Mjadala wa Mapendekezo ya Serikali Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi Kwa Mwaka wa Fedha 2017 / 18.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>