Published On: Mon, Jun 12th, 2017

MAPENDEKEZO YA KAMATI YA MCHANGA WA MADINI KWA SERIKALI

Share This
Tags

Kamati ya wachumi na wanasheria iliyowasilisha ripoti ya pili ya makontena ya mchanga wa madini Ikulu jijini Dar es salaam, imependekeza mambo kadhaa ya kuzingatiwa na serikali, benki kuu, na vyombo vya sheria.

Serikali imetakiwa kuendelea kuzuia usafirishaji wa makinikia mpaka kampuni za madini zitakapofuata sheria.

Kamati hiyo imependekeza serikali kuchunguza na kuchukua hatua kwa viongozi wa sekta mbalimbali za serikali wanaotoa leseni na wanaoongeza muda wa leseni, na walioondoa kwa makusudi nyaraka za usafirishaji wa makinikia.

Kamati imependekeza serikali kufuta utaratibu wa kupokea malipo ya mrahaba.

Imependekeza pia serikali kuchunguza mwendendo wa watumishi wa baraza la kodi.

Aidha kamati imependekeza sheria iongeze kiwango cha adhabu ya ukwepaji kodi.

Kamati imependekeza sheria iweke kiwango maalum cha umiliki wa hisa wa serikali.

Na imependekeza pia serikali iunde chombo cha kusimamia usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi.

= = =

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>