Published On: Fri, Jun 16th, 2017
Business | Post by jerome

MAKUBALIANO YA CHEMBA YA BIASHARA TANZANIA NA MIDITROV

Share This
Tags

URUSI ni Miongoni mwa Mataifa yanayofanya vizuri Duniani katika sekta ya Biashara na uwekezaji lakini pia Taifa hilo limepiga hatua kubwa katika kuimarisha mahusiano yake na baadhi ya Mataifa dhima kubwa ikiwa ni kuimarisha mikakati ya uwekezaji.

Ili kuweza kunufaika na kujifunza mbinu mbalimbali za kukuza biashara na kuendeleza sekta ya uwekezaji Chemba ya Biashara ya Dar es Salaam imeingia makubaliano na Chemba ya Biashara ya jimbo la DIMITROV lililopo nchini urusi. FRANCIS LUKWARO Ni mwenyrekiti wa Chemba ya Biashara ya Dar es Salama anaeleza kuhusu makubaliano hayo.

Makubaliano hayo yamelenga kugusa nyanja mbalimbali za kimaendeleo lakini tayari watendaji wa Chemba ya Biashara ya Dar es Salaam wanachakujivunia kupitia makubaliano hayo.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya jimbo la DIMITROV LUBOV DEMIDOVA amesema bara la Afrika lina rasilimali na fursa ntingi ambazo zinazkosa usimamizi na ungalizi hivyo wao kama chemba watajitahidi kuboresha mahusiano ili kusaidiana uzoefu wa kutumia vizuri rasilimali hizo.

Miongoni mwa Sekta ambazo zitanufaika na makubaliano hayo ni pamoja na sekta ya utalii,Kilimo,Ufugaji na Miundombinu ya uwezekaji wa sekta ya Viwanda .

= = =

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>