Published On: Wed, Jun 21st, 2017

Kiasi cha hekari 372,000 za Misitu huangamizwa kila mwaka nchini.

Share This
Tags

Serikali imesema kasi ya uharibifu wa misitu ni kubwa sana nchini ambapo kiasi cha hekari 372,000 za misitu huangamizwa kila mwaka kwa aina zote za uharibifu.

Ili kurejesha misitu nchiniĀ  katika hali yake ya kawaida inahitajika kupanda miti zaidi ya milioni 200 kila mwaka kwa mfululizo wa miaka 17.

Taarifa hiyo imetolewa Bungeni mjini Dodoma na naibu Waziri wa Maliasili na utalii Mhandisi RAMO MAKANI wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti maalum IMMACULATE SEMESI.

Katika hatua nyingine mbunge wa jimbo la morogoro kusini OMARY MGUMBA ameihoji serikali juu ya kuongeza ardhi kwaajili ya wakulima wadogo katika mradi wa Mkulazi ambapo naibu waziri wa kilimo mifugo na uvuvi WILIAM OLENASHA amesema swala hilo lipo katika utaratibu.

OLENASHA pia amesema kuwa serikali ina mpango wa kutoa elimu kwa vijana nchi nzima ili waweze kushiriki katika kilimo kwakujenga uchumi wa viwanda.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>