Published On: Wed, Jun 28th, 2017
Business | Post by jerome

Kenya:Maduka ya jumla ya Nakumatt yaendelea kusambaratika

Share This
Tags

Tangu kuanzishwa kwake mnamo 1987, kampuni hii inayomiliki maduka kadha nchini, imefurahia uthabiti na ufanisi mkubwa kibiashara.

Lakini uthabiti huo haupo tena kwani kufikia sasa Nakumatt inazongwa na mzigo wa madeni ya kima cha Sh15 bilioni, hali ambayo imelazimu kufungwa kwa baadhi ya matawi yake. Mfano ni kufungwa kwa tawi la barabara ya Ronald Ngala mwezi Februari mwaka huu.

Mwenendo wa baadhi ya wafanyakazi kushirikiana na wawasilishaji bidhaa kulipia bidhaa ambazo hazijawasilishwa, umetajwa kuwa mojawapo ya shida kubwa inayokumba Nakumatt.

Aidha, inadaiwa kuwa wakati mwingine wafanyakazi wa duka hili huagiza bidhaa ambazo hazinunuliwi kwa haraka.

Hali hiyo imewafanya maelfu ya wateja katika matawi yake 66 nchini Kenya, Uganda na Rwanda kukumbwa na uhaba wa bidhaa muhimu katika maduka hayo huku wafanyakazi wakiachishwa kazi.

Vile vile, kulingana na Shah, Halmashauri ya Ukusanyaji Ushuru (KRA) ilitoza Nakumatt faini ya Sh1 bilioni ambayo iliathiri shughuli za kampuni hiyo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>