Published On: Mon, Jun 12th, 2017

KAGERA WALIA NA UGONJWA WA MIGOMBA

Share This
Tags

Uchumi wa wananchi wa mkoa wa Kagera unazidi kuyumba kutokana migomba  kuendelea kushambuliwa na ugonjwa wa MNYAUKO BAKTERIA ambao unadaiwa kutokuwa na dawa mpaka sasa, pamoja na mabadiliko ya tabia nchi.

Kutokana na ugonjwa huo kuwa tishio kwa zaidi ya miaka kumi hadi sasa,wapo baadhi ya wakulima wa Migomba  walioamua kufyeka mashamba yao ya migomba na kuanza kulima mazao mengine kama walivyosikika wakielezea MARTHA VEDASTO na REHEMA KHARIDI wakazi wa Bukoba.

Kilio kikubwa kwa wakulima wa migomba ni kupata elimu kuhusiana na teknolojia mpya ya kilimo ili waweze kulima kisasa na kunufaika na kilimo cha Migomba.

Suluhu pekee ya kurejesha picha ya kijana iliyokuwepo hapo awali katika mkoa wa Kagera kutokana na ustawi wa Migomba, imeelezwa ni  kuanza kutumia Bioteknolojia mpya itakayosaidia upatikanaji wa miche bora ya migomba inayoendana na mabadiliko ya tabia ya nchi na kukinzana na magonjwa.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>