Published On: Sat, Jun 3rd, 2017
Sports | Post by jerome

JUVENTUS NA REAL MADRID KUCHUANA LEO

Share This
Tags

Mkufunzi mkuu wa Real Madrid Zinedine Zidane anakabiliwa na kizungumkuti cha kuamua nani kati ya Gareth Bale na Isco atacheza katika fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya leo.

Bale hajacheza tangu 23 Aprili lakini sasa yuko sawa kucheza.

Isco, ambaye alijaza pengo lake naye amekuwa akicheza vyema sana na amefunga mabao matano katika mechi nane walizocheza hivi karibuni.

“Wote wawili ni wachezaji muhimu sana na kila mmoja anaweza kutoa maoni yake lakini hilo halitaniathiri,” Zidane amesema.

Mkufunzi wa Juventus Max Allegri wachezaji wake wote pia wako sawa kucheza.

Gianluigi Buffon, Giorgio Chellini, Alex Sandro, Mario Mandzukic na Leonardo Bonucci walipumzishwa mechi ya mwisho ya Juve katika Serie A dhidi ya Bologna Jumamosi iliyopita.

Gianluigi Buffon, 39, atakuwa nahodha wa Juve katika mechi hiyo itakayochezewa Cardiff.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>