Published On: Mon, Jun 12th, 2017

JESHI LA POLISI MKOANI IRINGA LINAWASHIKILIA WATU SABA KUVAMIA NA KUJERUHI WACHIMBAJI TISA WA MADINI

Share This
Tags

Siku chache baada ya tukio la kuvamiwa na kujeruhi wachimbaji tisa wa madini katika mgodi wa Nyakavangala uliopo tarafa ya Ismani mkoani Iringa, Jeshi la polisi mkoani humo linawashikilia watu saba kwa tuhuma za kushiriki katika tukio hilo.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kushikiliwa kwa watuhumiwa hao Kamanda wa polisi mkoani iringa JULIUS MJENGI amesema mara baada ya kupokea taarifa hizo jeshi la polisi limefanya msako kuwatafuta watuhumiwa ambapo waliwakuta na silaha 1 aina ya Bastola inayodaiwa kutumika katika uvamizi huo.

Aidha kamanda MJENGI amethibitisha kutokea kwa ajali katika mgodi huo wa nyakavangala ambapo wachimbaji wadogo wa madini wamenusurika kufa mara baada ya kufunikwa na udongo katika shimo walilokuwemo majira ya saa tatu usiku ambapo tayari wachimbaji watatu wameokolewa wakiwa salama na mmoja bado anatafutwa.

Licha ya jeshi la polisi kufanya doria katika maeneo hayo bado changamoto kubwa inayotajwa ni uhaba wa mawasiliano yanayochangia kuchelewesha taarifa pindi kunapotokea tatizo ambapo wito umetolewa kwa serikali kuboresha mawasiliano katika eneo hilo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>