Published On: Mon, Jun 5th, 2017
Sports / World | Post by jerome

IS: TUNAHUSIKA NA SHAMBULIO LA LONDON

Share This
Tags

Polisi nchini Uingereza wamekuwa wakifanya msako kwenye makazi manne mjini London hadi usiku wa manane kama sehemu ya uchunguzi juu ya shambulio la Jumamosi ambapo watu saba waliuawa na wengine hamsini walijeruhiwa .

Wachunguzi wanajaribu kubaini endapo wanaume watatu waliendesha basi lao dogo na kuwagonga wapita njia kabla ya kuwachoma visu wengine wengi walipata msaada wowote.

Kundi la Islamic State limesema lilihusika na shambulio hilo.

Mwanamke mmoja raia wa Canada aliyeuawa katika shambulio hilo ametajwa katika vyombo vya habari.

Taarifa ya familia yake imesema alikuwa akifanya kazi katika hifadhi ya wasiokuwa na makazi kabla ya kuhamia Ulaya kuishi na mchumba wake.

Watu 21 waliojeruhiwa katika shambulio hilo wako mahututi.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>