Published On: Fri, Jun 2nd, 2017

DUNIA KUADHIMISHA WIKI YA MAZINGIRA

Share This
Tags

Kila jambo lina mwanzo wake,hii leo dunia imeanza kuadhimisha wiki ya mazingira yenye lengo la kuhamasisha kila mmoja kuchukua hatua kuhusu uharibifu  wa mazingira unaofanyika duniani.

Inaelezwa kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya uharibifu wa mazingira na umasikini, Kadri hali ya umasikini inavyoongezeka, ndivyo pia uharibifu wa mazingira unavyoongezeka.

Ni dhahiri kuwa siku za karibuni kumeshuhudiwa  ongezeko la uharibifu wa mazingira  linatokana na kuendelea kufyekwa kwa misitu, na kuharibiwa kwa vyanzo vya maji,na hii ndo hasara ambayo taifa hupata.

Huenda ukisikia uharibifu wa mazingira unawaza kuhusu misitu pekee lakini  unajua uhusiano uliopo kati ya maliasili na mazingira? Athari za mabadiliko tabia nchi  pia zimetapakaa katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Wakati tukiadhimisha wiki ya mazingira usisahau ofa ya kutembelea hifadhi za wanyama iliyotolewa na wizara ya maliasili na utalii.

Kila mwaka nchini takriban hekta 400,000 za misitu hupotea  kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo matumizi ya nishati ya kuni na mkaa.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>