Published On: Sat, Jun 17th, 2017

DC Ikungi aiomba serikali ifungie mgodi wa Shanta Mine

Share This
Tags

Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, imeiomba Serikali kuifutia leseni kampuni ya SHANTA MINE kwa kushindwa kufungua mgodi kwa zaidi ya miaka 14 sasa katika eneo la Mang’onyi, linaloaminika kuwa na utajiri mkubwa wa madini ya dhahabu.

Mkuu wa Wilaya hiyo, MIRAJI MTATURU ametoa ombi hilo baada ya kufanya ziara  kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu na kubaini tatizo lililopo kwa mwekezaji huyo.

Tangu mwaka 2003 kampuni hiyo imeshindwa kufungua mgodi kwenye eneo hilo huku Serikali ikiwa tayari imeipatia leseni, hali inayotia mashaka kwa wananchi.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>