Published On: Mon, Jun 19th, 2017

DAWA YA UKOKO KUPULIZWA MAJUMBANI GEITA

Share This
Tags

Takwimu za kidunia zinaonyesha kwamba wastani wa mtu mmoja hupoteza maisha kila dakika kutokana na ugonjwa wa Malaria.

Hii ni kwa mujibu wa Ripoti ya Shirika la Afya Dunani  (WHO) ya mwaka 2012.

Nchi zilizo na kiwango kikubwa cha ugonjwa huo ikiwemo Tanzania huchangia takribani asilimia 70 ya ukubwa wa tatizo hilo na kwamba akinamama wajawazito, watoto wenye umri chini ya miaka mitano pamoja na  wazee ni waathirika wakubwa wa ugonjwa huo.

Kutokana na hali hiyo halmashauri  ya Mji wa Geita kwa kushirikiana na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) na Shirika la kiserikali la ABT ASSOCIATES  wameanza kutekeleza zoezi la kupuliza dawa ya ukoko Majumbani katika halmashauri ya Mji huo, ikiwa ni mipango endelevu ya kitaifa ya kupambana na ugonjwa wa Malaria.

Tangu  mwaka 2010 mpaka sasa Mgodi wa GGM umekuwa ukishiriki zoezi hilo na umetumia takribani Bilioni mbili kwenye mapambano hayo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>