Published On: Sat, Jun 17th, 2017

Chama cha Mabaharia Tanzania champongeza Rais Magufuli

Share This
Tags

Chama cha Mabaharia Tanzania CMT kimepongeza harakati za utendaji kazi wa serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dokta JOHN MAGUFULI na kumuomba kurudisha upya wakala wa Meli nchini ili kulinda maslahi ya rasilimali za Tanzania.

Wakizungumza na CLOUDS FM wanachama hao wamepongeza hatua ya Rais Dokta MAGUFULI kwa kuunda tume iliyoleta matokeo chanya kwenye sataka la uchimbaji wa madini nchini

FRANK CHUMA ni mwenyekiti wa Mabaharia nchini, mbali na pongezi hizo amemshauri Rais MAGUFULI kukutana na wataalamu wa  masuala ya meli katika sekta yao.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo wa chama cha MABAHARIA ametoa ombi kwa Rais Magufuli kuanzisha wakala wa meli ili kulinda maslahi ya wazawa.

Nao baadhi ya wanachama wa chama hicho akiwemo SHIDA KILONGOLA na EMMANUEL MASAI hawakusita kuonesha furaha yao kuhusu utendaji kazi wa Rais magufuli na Serikali yake kwa kubeba mabango yenye ujumbe mbalimbali.

Matumaini ya Mabaharia hawa ni kuwa kile ambacho wamekishauri kitafanyiwa kazi na Seriali ya awamu ya tano ambayo siku zote imekuwa ni sikivu kwa Wananchi wake.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>