Published On: Sat, Jun 24th, 2017
Business | Post by jerome

Benki ya dunia yapongeza juhudi za Tanzania katika kupambana na ufisadi

Share This
Tags

Benki ya dunia imepongeza hatua zilizochukuliwa na Tanzania katika kupambana na rushwa nchini humo. Benki hiyo pia imetoa njia tano kwa Tanzania zitakazoongeza ufanisi kwenye vita hivyo badala ya kutegemea kuboresha sheria au kuwaanika hadharani watu waliohusika na ufisadi.Kwa mujibu wa mjumbe wa benki hiyo katika nchi za Tanzania, Burundi, Somalia na Malawi Bwana Bella Bird, mafanikio katika vita dhidi ya rushwa ni muhimu kwa maendeleo ya nchi inayopambana na umaskini.

Ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka 20 cha kupambana na rushwa cha benki hiyo wameshirikiana na nchi mbali mbali kupambana na rushwa na pia wamejifunza mengi ikiwemo haja ya serikali kuboresha motisha kwa wafanyakazi wake.Aidha Bwana Bird amesema Benki hiyo iko tayari kuisaidia Tanzania kupunguza ufisadi ili kuboresha utoaji wa huduma bora zitakazong’arisha maisha ya wananchi.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>