Published On: Wed, Jun 14th, 2017

Balozi wa Kuwait hapa nchini Jasem Al- Najem amemkabidhi Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan vifaa tiba vya uzazi.

Share This
Tags

Balozi wa Kuwait hapa nchini Jasem Al- Najem amemkabidhi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan vifaa tiba vya uzazi zaidi ya 200 ambavyo vitasambazwa katika hospitali mbalimbali kwa Tanzania Bara pamoja na Zanzibar.

Makabidhiano ya vifaa hivyo vya uzazi yamefanyika leo Ikulu ya Dar es Salaam ambapo Balozi wa Kuwait hapa Nchini Jasem Al- Najem amesema Serikali ya nchi hiyo imetoa vifaa hivyo kama hatua ya kuendelea kudumisha na kuendeleza mahusiano mazuri kati ya nchi hiyo na Tanzania.

Amesema kuwa Serikali ya Kuwait imetoa vifaa hivyo ikiwa ni awamu ya kwanza na lengo ni kutoa vifaa hivyo zaidi ya 1000 vyenye thamani ya shilingi milioni 40 kwa wanawake wajawazito na waliojifungua katika hospitali mbalimbali hapa nchini.

Mara baada ya kupokea msaada huo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameishukuru Serikali ya Kuwait kwa msaada huo na amesema utasaidia sana wanawake wajawazito na waliojifungua kupata vifaa vya uzazi ambavyo vinahitajika wakati mwanamke mjamzito anapojifungua na baada ya kujifungua.

Makamu wa Rais pia amesisitiza kudumishwa kwa mahusiano mazuri yaliyopo kati ya nchi ya Kuwait na Tanzania kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa pande zote Mbili.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>